Siwezi kusubiri kuacha wazimu wa mitandao na kuzingatia Mungu na familia-Amberay akiri

Muhtasari
  • Yeye ni mshawishi wa kweli kwenye mitandao ya kijamii na balozi wa chapa ambaye anafanya kazi nzuri katika hilo
  • Amber Ray ni mama wa mtoto mmoja wa kiume ambaye pia anampenda sana

Mwanasosholaiti maarufu Amber Ray kwa sasa yuko Mombasa ambako anafurahia likizo yake pamoja na familia yake.

Yeye ni mshawishi wa kweli kwenye mitandao ya kijamii na balozi wa chapa ambaye anafanya kazi nzuri katika hilo.

Amber Ray ni mama wa mtoto mmoja wa kiume ambaye pia anampenda sana.

Amekuwa akigonga vichwa vya habari mwaka jana alipokuwa kwenye uhusiano na mfanyabiashara Jimal Roho Safi.

Uhusiano au ndoa yao hakudumu kwa muda mrefu, kwani wawili hao waliachana huku JImal akioekana kumrudia mkewe Amira, ambaye baada ya miezi michache alisema kwamba anataka talaka.

Pia, wawili hao wameonekana wakiwa pamoja mara kadhaa hata baada ya kuwaambia na kuwathibitishia mashabiki wao kuwa wametengana.

Akiwa likizoni, alijibu kwenye chapisho kuhusu jinsi watu wanavyoweza kulia kwenye kamera.

"Siwezi kusubiri kuacha wazimu huu wa mitandao ya kijamii na kuzingatia wapendwa wangu, biashara, Mungu na familia," Alikiri Amberay.