Wakati mwingine siwezi kumudu kodi ya 2,500-Manzi wa Kibera afunguka

Muhtasari
  • Manzi wa Kibera alionyesha nyumba yake ya udongo iliyoko katika eneo la Ayany, Kibera
Mwanasoshalaiti Manzi wa Kibera
Mwanasoshalaiti Manzi wa Kibera
Image: Instagram

Mwanasosholaiti Manzi wa Kibera almaarufu Wambui amefunguka kuhusu matatizo yake ya kifedha, na jinsi yamemfanya kuwa kicheko kwenye mitandao ya kijamii.

Katika mahojiano na Nicholas Kioko, Manzi wa Kibera alionyesha nyumba yake ya udongo iliyoko katika eneo la Ayany, Kibera.

“Sioni aibu, mwanzo sikutaka hata watu wajue mahali ninapokaa. Sasa hivi nimezoea, mtu yeyote anaweza kunitembelea," Manzi wa KIbera alisema.

Manzi wa Kibera alisema hawezi kuhama kutoka chumba kimoja hadi kikubwa zaidi kwa kuwa hana uwezo wa kulipa karo zaidi.

"Kama mtu anaweza kunisaidia basi ni sawa. Lakini nisingependa kujisumbua na kupanga nyumba ya chumba kimoja. Wakati mwingine siwezi kumudu 2500 (kodi ya sasa) nitaendaje kwenye nyumba elfu 5,000? Watu walikuwa wakinidhulumu mtandaoni, wakisema najifanya bado ninaishi ghetto. Ningependa kuondoka katika nyumba hii," Manzi wa Kibera alisema huku akitokwa na machozi.