Salaale! Mchungaji awaosha washirika wa kike wa kanisa lake ili kuwatakasa

Muhtasari

•Inaripotiwa mtumishi huyo aliwaosha washirika wa kike wa kanisa lake kuwatakasa ili waingie mwaka wa 2022 wakiwa watakatifu.

Mhubiri aosha washirika wake
Mhubiri aosha washirika wake
Image: HISANI

Mhubiri mmoja kutoka Ghana amekuwa gumzo mitandaoni kwa kipindi cha siku tatu ambacho kimepita baada ya video inayoonyesha  akiosha wanawake katika kanisa lake kuvuja kwenye mitandao ya kijamii.

Katika video zinazosambazwa mitandoni, mhubiri huyo ambaye jina lake halijatajwa pia alionekana akinyoa sehemu za siri za washiriki wa kike wa kanisa lake mkesha wa mwaka mpya.

Kwa mujibu wa ripoti zilizosambazwa kwa wingi kutoka nchi hiyo ya Afrika Magharibi, 'mtumishi huyo wa Mungu' aliwaosha waumini wa kike akiwatakasa ili waingie mwaka wa 2022 wakiwa watakatifu bila doa la dhambi.

Video zinazosambazwa zinaonyesha waumini wa kike wakienda mbele ya kanisa na kuvua nguo zao kuingia ndani karai iliyotiwa maji. Baada ya hilo kufanyika mhubiri huyo anaonekana akichukua kitambaa na kuanza kuwaosha.

Baada ya mchungaji kuridhika kuwa mshiriki anayeoshwa ni safi anaonekana akiwaelekeza kwa mwanamke mwingine aliyesimama karibu ambaye aliwapangusa kwa kitambaa kilichokauka.

Baadhi ya wanawake walionekana wakisimama mbele ya mhubiri huyo na kuvua chupi na mhubiri huyo akichukuwa wembe na kunyoa sehemu zao za siri.

Maajabu haya kweli!