'Naumwa jamani,'Ujumbe wa Fahyvanny uliowaacha mashabiki na maswali mengi

Muhtasari
  • Ujumbe wa Fahyvanny uliowaacha mashabiki na maswali mengi
  • Hii ni baada ya kusema kuwa anateseka kwenye chapisho lake la hivi punde ambalo limesambaa mitandaoni

Baby mama wa Rayvanny Fahyvanny ameacha maswali miongoni mwa wanamitandao kwenye mitandao tofauti ya kijamii.

Hii ni baada ya kusema kuwa anateseka kwenye chapisho lake la hivi punde ambalo limesambaa mitandaoni.

Kulingana na chapisho hilo ambalo Fayhma aliisambaza kupitia akaunti yake ya Instagram, mwanadada huyo alikuwa akiwaambia wanamitandao kuwa anaumwa sana, jambo ambalo watumiaji wa mitandao hawawezi koma kulizungumzia.

"Naumwa jamani!" Ameandika Fayhma.

Sasa kauli hii ya hivi punde zaidi ya Fahyvanny akisema kwamba anaumwa imeenea kwenye mitandao tofauti ya kijamii ambapo, inazua hisia tofauti kwa sasa.

Wengi wako tayari kumuuliza Fahyvanny kwa nini anaumwa huku, wengine wako nje wakitoa hisia za kuchekesha kuhusu taarifa ya Fahyvanny kwa wakati mmoja.

Msanii Rayvanny na Fahyvanny walitengana mapema mwaka jana huku kutengana kwao kukizua mdahalo mitandaoni.