Tristan Thompson akiri ndiye baba wa mtoto wa Maralee Nichols

Muhtasari

•Thompson ambaye ni  baba wa watoto watatu  kupitia ukurasa wake wa Instragram alieleza wazi kuwa yeye ni baba mtoto wa kiume aliyezaliwa hivi karibuni na mwanamke kutoka Huston

• Aliomba msamaha kwa mpenzi wa zamani  na mama wa watoto wake, Khloe Kardashia 

Tristan Thompson
Tristan Thompson
Image: Hisani

 Nyota wa NBA, Tristan Thompson mwenye umri wa miaka 30 siku ya jumatatu alikiri ndiye Baba wa mtoto wa Maralee Nichols aliyezaliwa tarehe 1 Disemba.

Thompson ambaye ni  baba wa watoto watatu  kupitia ukurasa wake wa Instragram alieleza wazi kuwa yeye ni baba mtoto wa kiume aliyezaliwa hivi karibuni na mwanamke kutoka Huston baada ya kupata matokeo ya mtihani wa uzazi.

Isitoshe aliomba msamaha kwa mpenzi wa zamani  na mama wa watoto wake, Khloe Kardashia 

  "Ninawajibika kikamilifu kwa matendo yangu. Kwa kuwa sasa ubaba  umeanzishwa, natarajia kumlea mtoto wetu kwa amani. Ninaomba radhi kwa kila mtu niliyemuumiza au kumkatisha tamaa katika kipindi chote hicho" alinakiri

 Isitoshe alielekeza ujumbe kwa Khloe, ambaye amepata  mtoto wa kike  naye huku  akisema, "Hustahili maumivu ya moyo na fedheha niliyokusababishia. Hustahili jinsi nilivyokutendea kwa miaka mingi. Matendo yangu yamekusaidia. hakika hauendani na jinsi ninavyokuona."

Alimumiminia ujumbe wa kuonyesha mahaba kwake kwa kusema "Nina heshima na upendo mkubwa kwako. Bila kujali unachoweza kufikiria. Tena, samahani sana."