Eric Omondi atoa maagizo kwa Mapromota

Muhtasari

•Pendekezo kwa mapromota na waandalizi wa  matashamasha mbalimbali mwaka 2022.

•Mcheshi huyo ambaye aliweka wasanii katika daraja mbili, ambazo  ni daraja la kwanza(A) na daraja la pili(B).

Eric Omondi
Eric Omondi
Image: INSTAGRAM// ERIC OMONDI

Mchekeshaji maarufu Erick Omondi Jumanne alitoa pendekezo ambalo mapromota wa humu nchi wanafaa kufuata wakati wanafanya maandalizi ya matamasha mbalimbali 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Omondi alitoa taarifa kwamba mapromota na waandalizi wa  matamasha mbalimbali wamekuwa wakiwanyanyasa wasanii kwa malipo duni ilhali wakiwalipa wasanii wa nje donge nono 

Mcheshi huyo ambaye aliweka wasanii katika daraja mbili, ambazo daraja la kwanza(A) na daraja la pili(B) 

Kikundi cha kwanza(A) kinachohusisha Nadia Mukami, Khaligraph Jones,Otile Brown, Nyashinski  na Sauti sol. Alisema wasanii wakikundi hicho  hawafai kulipwa chini ya 600,000 kwa kila tamasha watakaoudhuria humu nchini

Kikundi cha pili(B)  alisema nacho hakifai kulipwa chini ya 450,000 huku akitaja Ethic, Trio mio ni baadhi  ya wasanii walio kwenye kikundi hicho.

Aidha, Omondi amesema wasanii wote watakaoalikwa kutumbuiza kwenye tamasha yoyote  ni lazima mapromota wawalipe kiasi cha pesa kisichopungua asilimia 75 ya kiwango cha pesa waliokubaliana kabla ya siku ya kutumbuiza na salio walipe siku ya tokea husika

"Tafadhali TAARIFA kuwa MWAKA huu  mimi BINAFSI NITACHUNGUZA kwa  undani kwa Kila TUKIO!!! Nataka kujua WASANII wanalipwa kiasi gani." Omondi alisema

 Isitoshe alieleza "Ninataka kuhakikisha kuwa Kila MSANII analipwa ASILIMIA 70 ya pesa zake KABLA na ASILIMIA 30 siku ya Tukio kabla ya TUKIO."