"Sikuwa nataka kutumia mtu!" Baba Gloria afunguka kuhusu skendo ya ujumbe mchafu aliotuma WhatsApp

Muhtasari

•Alisema kikundi cha WhasApp ambacho alituma picha kilikuwa kimeundwa ili kuchangisha pesa za kuandaa mazishi ya ndugu ya mwanasiasa mmoja mkubwa eneo hilo.

•Baba Gloria alieleza kwamba sticker hiyo ilikuwa imetoka kwa kikundi kingine cha WhatsApp ambacho kilikuwa na watu wenye tabia  tofauti, zingine ambazo sio za kupendeza.

Leonard Githinji almaarufu kama Baba Gloria
Leonard Githinji almaarufu kama Baba Gloria
Image: YOUTUBE// MPASHO

Hatimaye Leonard Githinji Mugendi almaarufu kama Baba Gloria ambaye alivuma sana  kote nchini mnamo mwezi Oktoba mwaka uliopita baada ya ujumbe mchafu aliokuwa ametuma kwa kikundi cha WhatsApp kusambaa mitandaoni amefunguka kuhusu yaliyojiri wakati ule.

Akiwa kwenye mahijiano na Mpasho, Baba Gloria alikiri alituma sticker hiyo chafu kimakosa  kwa kikundi cha WhatsApp cha kuchangisha pesa za mazishi kisha akaweka simu kando kwani hakugundua limetendeka.

Baba huyo wa watoto wawili alifichua kwamba baada ya kosa hilo kufanyika mwana wa marehemu ndiye alimpigia simu dakika chache baadae kumjulisha kilichokuwa kimetendeka na akamuomba aifute sticker ile haraka.

"Nikiwa kwa kikundi siku moja nikiwa napata chakula cha mchana  nikaingia WhatsApp Group hiyo ndio niangalie vile watu wanaendelea kuchanga. Nilipopigiwa simu nirudi kazini hapo ndipo nilichukua simu niweke kwa mfuko. Nilipokuwa naiweka kwa mfuko ile sticker ikajituma kwa kuwa ile WhatsApp group ilikuwa imefunguka na nilikuwa nimewasha data. Kijana ya mwenye alikuwa ameaga akanipigia akaniambia kuna kitu nilikuwa nimetuma kwa kikundi na akaniomba nifute haraka. Nikaingia WhatsApp haraka alafu nikafungua group nikafuta haraka" Baba Gloria alisimulia.

Mfanyibiashara huyo kutoka Embu alisema kikundi cha WhasApp ambacho alituma picha kilikuwa kimeundwa ili kuchangisha pesa za kuandaa mazishi ya ndugu ya mwanasiasa mmoja mkubwa eneo hilo.

Alisema kwa bahati mbaya kabla hajafanikiwa kufuta sticker chafu ambayo alikuwa ametuma tayari kuna mmoja wa waliokuwemo ambaye alikuwa amechukua screenshot na kuisambaza.

Baba Gloria alieleza kwamba sticker hiyo ilikuwa imetoka kwa kikundi kingine cha WhatsApp ambacho kilikuwa na watu wenye tabia  tofauti, zingine ambazo sio za kupendeza.

"Sikujua kuna mtu alikuwa amescreenshot. Hapo ndipo nikaanza kupigiwa simu na kutumiwa jumbe watu wakitaka kunijua. Niko kwenye makundi mengi kwa simu yangu na sio watu wote waaminifu. Kuna kikundi kimoja ambacho kilikuwa na mtu ambaye alikuwa anatuma stickers. Akizituma pale kwa kikundi zilikuwa zinakuja kwa simu. Sikuwa najua kwamba kuna mtu ashazituma. Hata mimi sikuelewa kilichotendeka ikajitoa pale na kujituma. Sikuwa nataka kutumia mtu, nilijipata imeenda" Alisimulia.

Alisema kwamba hakufikiria ingetokea kuwa suala kubwa na alishangaa sana kuona ikisambaa mitandaoni.

Pia  alikiri kwamba baada ya hilo kufanyika alipoteza baadhi ya marafiki ba vilevile akapata marafiki wengine wengi wapya