Burna Boy Anunua Gari la kifahari

Burna Boy
Image: Hisani

Mwanamuziki kutoka nchi ya Nigeri, Ebunoluwa Oguru almaarufu  Burna Boy,amejipatia zawadi  la  Gari la kifahari aina ya Lamborgin 

Burna Boy, ambaye ni mshindi wa  tuzo za Grammy  mwaka  jana, amenunua gari hilo ambalo lilitengenezwa Urusi mwaka wa 2022

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Burna Boy alionyesha picha ya gari hilo la kisasa na ambapo mashabiki wake walipongeza 

Msanii huyo wa kibao cha 'On The Low' alituma habari kwa  Lewis Hamilton akimjuza   kwamba ako njiani  gari jipya.

Aliendelea kusema anawatakia familia yake heri ya mwaka mapya na kuwaonyesha gari hilo jipya la kisiasa huku akiliendesha kwa mwendo wa upesi.

"Heri ya Krismasi na Mwaka Mpya, Damini. Mungu anakupenda, familia yako inakupenda na mimi nakupenda. Huna haja ya kitu kingine chochote. Toleo la Novitec la 2022. Mwanachama mpya zaidi wa familia ya Lamborghini." Burna Boy alisema