Nadia Mukami afichua kuharibikiwa na mimba huku akijibu madai ya kuwa mjamzito

Nadia MUkami
Image: Hisani

Mwanamuziki Nadia Mukami amejitokeza kuelezea kinagaubaga kuhusu madai yake kuwa na ujauzito.

Alhamisi aliweka kanda  ya video kwenye ukurasa wake wa Instagram huku akimwelekeza kidole cha lawama Jalang'o.

 Hii ni kufuatia kauli ya mcheshi Jalang'o, kwamba Nadia ajitokeze na kueleza wazi kuwa hivi karibuni anatarajia kifungua mimba.

Kauli yake mcheshi huyo haikuchukuliwa vyema na wapenzi hao wawili, huku wakimkejeli Jalang'o kwa matamshi yake, na kusema hakufanya vyema kuingilia maisha ya wenyewe.

Alhamisi mwanamuziki Nadia amejibu na kueleza kero lake nakusema Jalang'o alijihusisha na mambo yasiyo mhuhusu huku akisimulia siku ambayo walienda kumtembelea kwake nyumbani

"Ulipaswa kuchukua simu yako na kumuuliza Arrow Bwoy... kwa sababu huwezi kujua kwa nini watu hufanya mambo fulani Kama ni ukweli, namaanisha, watu wamekuwa wakizungumza, watu wamekuwa wakitutukana na hatujali kwa sababu mimi na yeye .. tunajua ukweli

Arrow Bwoy hajui vita, aliwapoteza watu wawili maishani mwaka mwaka jana baba yake na Safari," Alizungumza Nadia.