Akaunti ya Instagram ya Edgar Obare ya yasitishwa

Muhtasari
  • Akaunti ya Instagram ya Edgar Obare ya Instagram yafutwa
  • Pia mwaka jana Edgar alipata pigo kubwa baada ya akaunti yake rasmi ya Instagram kufutwa baada ya kufichua vipindi vya 'Wash Wash'
Edger Obare
Edger Obare
Image: Hisani

Mwanablogu Edgar Obare Ijumaa alipasua mbarika kwamba akaunti aliyokuwa akimiliki ya Instagram imefutwa.

Obare, kupitia ukurusa wake wa Twitter aliwaeleza Wakenya kwamba akaunti yake ya Instagram BNNKe imefutwa na hajapata kiini cha kufutwa kwake.

Wakenya waliamshwa na habari hizo wengi wakijiuliza ni kwa nini  Akaunti yake itupiliwe mbali .

Obare alijitokeza wazi na kueleza taarifa hio kupitia ukurasa wa Twitter.

"Habari za asubuhi,  instagram leo imeamua kuzima akaunti yangu ya bnnke  . Tunajitahidi kutafuta la kufanya baadaye, tunapokata rufaa dhidi ya uamuzi wa Instagram, hivi karibuni tutakuwa pamoja" Obare alidokeza kwenye ukarasa wake wa Instagram. 

Meta ambayo ni kampuni kuu ya Instagram imekuwa na msimamo mkali  linapokuja suala la kuzima akaunti  ambazo hazifuati kanuni ambazo zimeweka na kampuni hio.

Mnamo Septemba mwaka jana, kampuni hiyo ulichocheshwa na maseneta wa Marekani kuhusu Program  zake kwa watumiaji wachanga zaidi.

Hii ilitokana na ripoti iliyoonyesha kuwa kampuni hiyo inafahamu kuwa Instagram inayomilikiwa na Meta inaweza kuwa na athari  kwa vijana  wachanga.

"Sasa tunajua kwamba Instagram mara kwa mara hutanguliza faida badala ya usalama wa mtandaoni wa watoto. Tunajua inachagia ukuaji wa bidhaa zake badala ya ustawi wa watoto wetu...Na sasa tunajua kuwa haina utetezi katika kuchukua hatua ili kuwalinda," Seneta wa chama cha Democratic Richard Blumenthal alisema.

Pia mwaka jana Edgar alipata pigo kubwa baada ya akaunti yake rasmi ya Instagram kufutwa baada ya kufichua vipindi vya 'Wash Wash'.