•Sophie Momodu, ambaye ni mama mzazi wa mtoto wa kwanza wa msanii maruufu nchini Nigeria, Davido
•Sophia Momodu alisema ashamaliza kukaa kimya kuhusu kile wanamitandao wanakichapisha kumhusu yeye
Mpenzi wa zamani wa msanii Davido, Sophie Momodu amejitokeza na kueleza bayana kuhusu watu wanaomsumbua mtandaoni kwa kucheza na hisia zake
Sophie Momodu, ambaye ni mama mzazi wa mtoto wa kwanza wa msanii maruufu nchini Nigeria, Davido. Kupitia ukurasa wake wa Instagram alitokwa na chozi huku akieleza kero wanamitandao wamekuwa wakieneza uvumi kwa mitandao kwa mambo wasioyajua.
Sophia Momodu alisema ashamaliza kukaa kimya kuhusu kile wanamitandao wanakichapisha kumhusu yeye.Alionyesha kukasirishwa na kundi la watu linalomuandama kwa kuonekana kumuunga mkono baba ya mtoto wake
Akizungumza kuhusu tuhuma za kuwa na marumbano na mwanamke anayesemekana ni mama wa mtoto wa pili wa Davido. kwa mujibu wake alidai. alitumia miaka sita iliyopita kupambana na watu mitandaoni ambao hawajawi kuona lolote jema kumhusu yeye.
"Imekuwa miaka 6 ya kumtukana Sophia. imetosha. Niacheni," alisema
Aidha, alisema anachojaribu kufanya ni kumlea binti yake kuhakikisha ana husiano mwema na babake yake. alitimiza kwa kusema mwaka huu mpya wa 2022, hutofumbia macho yeyote atayeeneza uvumi juu yake hasa utakaohusisha mzazi mwenza.
.