• Staa wa Bongo wa mtindo wa Singeli, Dulla Makabila amejitokeza wazi na kumweleza The African Princes almaarufu Nandy kwamba anataka wafanye Kolabo.
Staa wa Bongo wa mtindo wa Singeli, Dulla Makabila amejitokeza wazi na kumweleza The African Princes almaarufu Nandy kwamba anataka Kolabo naye.
Dulla, ambaye alipakia video kwenye ukarasa wake wa Instagram, akiwa kwenye tamasha za kufunga mwaka Nandy, alieleza anatamani kufanikisha malengo yake kufanya kazi ya muziki pamoja na Nandy.
"Hongera Sana Mwanangu Umeua Mnoo Naamini Kwenye Uwezo Wako Kuna Haja ya Kufanya Kitu Naomba simamia Hili Mashabiki Wa Singeli Wamependezewa Na Anachokifanya Mrs Billnass
Nandy, ambaye ni msanii kutoka nchi ya Tanzania, vile vile muigizaji kwenye mojawapo ya kipindi sifiki nchini Tanzania alionekana kupendezwa na pendekezo hilo la Makabila. Alitumia sehemu ya maoni ya Makabali kuonyesha ni pendekezo nzuri huku akitumia alama ya moto kuthibitisha ameona.
Kilichosalia ni kwa Meneja wanaosimamia kazi ya Nandy kupanda wakati wa kutimiza pendekezo hilo la Mwanamuziki maarufu wa Singeli, Makabali