Najutia wakati nilikuwa maarufu,'Manzi wa Kibera asema baada ya madai amekuwa akiwadanganya Wakenya

Muhtasari
  • KUlingana na mwanasosholaiti huyo anajutia siku ambayo alikuwa maarufu kwani maisha yake yalizidi kuwa magumu
Manzi wa KIbera
Image: maktaba

Mwanasosholaiti chipukizi Manzi wa Kibera kwa mara nyingine amekanusha madai kwamba amekuwa akiwadanganya Wakenya kwamba anaishi maisha ya umaskini.

KUlingana na mwanasosholaiti huyo anajutia siku ambayo alikuwa maarufu kwani maisha yake yalizidi kuwa magumu zaidi.

"Kwa hiyo mimi naishi poa na najifanya ati naishi kibera? Mimi mwenye christmas nilikula chapati na ndengu na tarehe 26 ndio rafiki yangu alinitumia pesa coz nili mlilia kwa simu.

Naweza hata kumtaja akikubali.najuta siku nilikua maarufu kwani ndio siku niliacha hawking mjini. watu walianza kuniona hivyo maisha yangu yakawa magumu na magumu na wakati mwingine nililala njaa na wakati huo huo kutrend.Nilifanya show za moja kwa moja kwenye video za whatsapp ili kuhudumia," Alisema Manzi wa Kibera.

Pia aliwashukuru wote ambao walimsaidia baada ya kuhitaji msaada wao, na kusema kwamba hivi karibuni ataenda nchi za nje.

"Lakini asante kwa wote waliokuja kwa ajili yangu kwa sababu karibuni sana ndakua na passport.Yes Germany inaeza kubali kwenda visa ama ikatae but heri niende ata Saudi nioshe viombo kuliko kufanya interview za youtube ambazo hazini saidi and at the end natukanua nikakama mimi si mtu....thanks so much nicholas am grateful na siku moja I'll surprise you God willing. . '