Aliiba zaidi ya elfu 500,000,'Obidan Dela afichua sababu kuu ya kuachana na Manzi wa Kibera

Muhtasari
  • Manzi Wa Kibera kwa sasa anavuma mtandaoni kutokana na madai kadhaa. Mungai eve tayari amemuweka wazi kwa kughushi maisha yake duni, ili Wakenya wampe pesa
Mwanasoshalaiti Manzi wa Kibera
Mwanasoshalaiti Manzi wa Kibera
Image: Instagram

Manzi Wa Kibera kwa sasa anavuma mtandaoni kutokana na madai kadhaa. Mungai eve tayari amemuweka wazi kwa kughushi maisha yake duni, ili Wakenya wampe pesa.

Aliyekuwa mume wa zamani wa Manzi Wa Kibera, tajiri Obidan Dela, amefichulia umma, sababu kuu iliyomfanya aachane na Manzi Wa Kibera.

"Nilipatana na Manzi wa Kiera katika kipindi cha wife material, nilimtumia ujumbe baada yake kusema kwamba anamtafuta mwanamume, tulioana na nilimpenda sana 

Ni mrembo ambaye anasema uongo, lakini anapaswa kujua kile anahitaji maishani mwake, kuna nafasi yake kurudi kwani bado nampenda, sisi ni binadamu na kweli huwa tunateleza," Alisema Obidan.

Akizungumza katika mahojiano na mtangazaji Ali, Obidan alisema kuwa Manzi Wa Kibera alikuwa mke wa nyenzo, na alikuwa mzuri katika kupika na pia kitandani, lakini sababu kuu iliyomfanya kuachana naye, ilikuwa kwamba Manzi Wa Kibera alikuwa mwizi.

Obidan alisema kuwa Manzi Wa Kibera alimwibia  zaidi ya ksh 500,000, na hii ilimfanya kuachana naye.

Hata hivyo Obidan alisema kuwa yeye ni msichana mzuri na anajua kufanya kazi za nyumbani na haswa kupika.

" Alichukua pesa nyingi zaidi ya elfu 500,000,nakumbuka kuna wakati tulikosana kurudi nilimpata amevunja vitu kwa nyumba hata televisheni

Mimi nilimsamehe kwa yote ambayo alinifanyia, na kama nilimkosea pia anapaswa kunisamehe, lakini ajue kwaba sio kila siku wakenya watakusaidia

Ajifunze kuwekeza, naamini ni mrembo ambaye anaweza fanya biashara na kuwa bilionea."

#presenterali