Niko 'single'-Zuchu afunguka kuhusu uhusiano wake na Diamond

Muhtasari
  • Zuchu afunguka kuhusu uhusiano wake na Diamond
  • Staa wa Bongo Diamond hakujitokeza na kuzungumzia madai hayo, huku Zuchu akizungumzia alikana kwamba wawili hao ni wapenzi
Diamond Platnumz na Zuchu
Diamond Platnumz na Zuchu
Image: INSTAGRAM

Msanii wa ike kutoka Tanzania Zuchu na staa wa bongi Diamond Platnumz walivuma sana wiki jana mitandaoni baada ya madai kuwa wanachumbiana.

Staa wa Bongo Diamond hakujitokeza na kuzungumzia madai hayo, huku Zuchu akizungumzia alikana kwamba wawili hao ni wapenzi.

Kulingana na Zuchu amekuwa 'single' kwa zaidi ya mwaka mmoja na bado yuko 'single'.

"Niko single, ukweli ni kuwa nimekuwa single kwa muda mrefu karibu mwaka mmoja , mahusiano mengi ambayo hufanyika kwa haraka, huwa hayakamiliki vyema

Nangoja wakati ufaao ili niweze kuchumbiana lakini kwa sasa sina nia," Alisema Zuchu.

Alipokuwa kwenye mahojiano na Mbengo TV, Bi Kopa alipuuzilia mbali madai hayo huku akisema alishtuka sana uvumi kuhusu mahusiano ya bintiye na Diamond ulipovumishwa mitandaoni.

Kopa alisema aliwasiliana na bintiye na akamueleza hali halisi kuwa huo ni uvumi tu usio na msingi. Zuchu alimhakikishia mamake kuwa Diamond amekuwa akionyesha heshima kubwa kwake na hakuna chochote kinachoendelea kati yao.

"Wakati ule Zuhura aliniambia Diamond anamheshimu sana na hajawahi hata siku  moja kuniambia vitu vya kipuzi. Nilishtuka maanake watu walikuwa wanavumisha kupita kiasi. Nilishangaa mbona walivumisha kupita kiasi. Mimi mwenyewe sikushughulika sana. Nilimuuliza Zuhura mbona watu walivumisha sana ama kuna kitu chochote. Aliniambia hamna wala hajawahi kuvunjiwa heshima hata siku moja. Mimi nilichukulia kama kitu cha kawaida" Alisema Khadija Kopa.