'Esther Musila si dada yako au mama yako,'Ringtone amkashifu Andrew Kibe

Muhtasari
  • Guardian Angel na Esther ni watu wawili wanaopendana. Wana zaidi ya miaka 18 na wanaweza kufanya chochote wanachotaka. Sioni tatizo kwao kuolewa
Guardian Angel, Esther Musila
Guardian Angel, Esther Musila
Image: INSTAGRAM

Mwimbaji wa nyimbo za injili,Ringtone amemkashifu Andrew Kibe kwa kumkosoa Guardian Angel baada ya kufunga pingu za maisha na Esther Musila.

Guardian Angel na Esther  wamekuwa kwenye mahusiano kwa takriban miaka 18 na wameweza kufunga ndoa mwaka huu. 

Kupitia  kwenye ukurusa wake wa instragram, Ringtone amechapisha  kanda la video kumkosoa Kibe kwa kauli aliyoitoa kwa wapenzi hao.

"Guardian Angel na Esther ni watu wawili wanaopendana. Wana zaidi ya miaka 18 na wanaweza kufanya chochote wanachotaka. Sioni tatizo kwao kuolewa.Zaidi ya hayo Guardian hajaoa mwanamume mwenzake bali mwanamke mrembo."

Aliongeza kwamba anapendelea ndoa ya ao wawili pia kuwapongeza kwa maamuzi waliofanya ya kuwa mume na mke."Esta angenikaribia na kusema ananipenda, ningemuoa pia. Hongera Guardian Angel"

Kwa Andrew Kibe alimwambia kwamba anashindwa mbona aingilie ndoa ya Guardian

"Kwa Andrew Kibe, Esther Musila si dada yako au mama yako, Guardian Angel pia si ndugu yako au jamaa yako kwa hiyo una shida gani? Una uchungu sana, ni kana kwamba ulitaka Esther aolewe na wewe ama Mlezi Angel akuowe"