Nick Ndeda azungumzia madai ya kuachana na Betty Kyallo

Muhtasari
  • Nick Ndeda azungumzia madai ya kuachana na Betty Kyallo

Kwa siku chache zilizopita uvumi umekuwa ukienea kwamba mjasirimai na mtangazaji Betty Kallo ameachana na mpenzi wake Nick Ndeda.

Wawili hao hawakujitokeza wazi wazi na kuzungumzia uvumi huo ulioenea mitandaoni.

Ndenda akizungumza na mpasho, amezungumzia madai hayo huku akisema kwamba wao ni marafiki na Betty na mambo hayatabadilika.

"Tulifurahia uhusiano mwema na wa ajabu, lakini bado tunachambua mambo,sisi ni marafiki wazuri," Alizungumza Ndeda.

Uhusiano wao ulifahamika kwa umma JUlai mwaka jana, huku baadhi ya mashabiki wakiamini kwamba wawili hao watavuka ng'ambo nyingine na kufunga pingi za maisha.

Betty amebarikiwa na mtoto mmoja ambaye amekuwa akionyesha upendo wake kwake.

Pia ni mama ambaye ana urembo wa kipekee, na amependwa na asilimia kubwa ya wanamitandao mitandaoni.