Diamond, Zari ajivunia mtoto wao Tiffah baada ya kuhitimu

Muhtasari

•Mwaka 2022 nilianza na mahafali ya mwaka jana ambayo hayakufanyika mwaka jana kwa sababu ya idadi kubwa ya virusi vya Corona

Diamond na mwanawe Tiffah Princess
Diamond na mwanawe Tiffah Princess
Image: Instagram/Diamond Platnumz

Diamond Platnumz ameonyesha furaha kubwa baada ya mtoto wake wa kwanza wake kike Tiffah Princess kuhitimu kuingia darasa lingine.

Tiffah mwenye umri wa miaka 6 ameingia daraja la kwanza  mwaka huu, baada ya kuhitimu kwenye shule moja ya kifahari huko Afrika Kusini. 

 Kupitia ukurusa wake wa Instagram, Tiffah Princess  amechapisha ujumbe wa kuonyesha furaha yake hasa wakati huu wa janga la Corona.

"Mwaka 2022 ulianza na sherehe ya kufuzu kwangu hafla ambayo haikufanyika mwaka jana kwa sababu ya idadi kubwa ya virusi vya Corona... lakini niko hapa sasa. Home girl amehitimu na kuingia darasa la juu," aliandika Tiffah

Baada ya mashabiki wa Tiffah kumpongeza,Diamond alichapisha picha yake kwenye ukurasa wake  wa instagram ikiambatanisha na ujumbe kwamba anajivunia kuwa baba wa mtoto huyo.

Diamond na mpenzi wake wa zamani Zari Hassan wana watoto wawili ambao ni Princess tiffah na  Prince Nillian,wote wanaishi na mama yao nchini Afrika kusini.

Mama wa Diamond pia hakuachwa nyuma kummiminia  mjukuu wake pongezii ambapo alichapisha kanda za video akiwa na binti huyo.  Mashabiki nao hawakuficha furaha yao huku wakimtumia ujumbe wa heri njema.