'Masomo sio kila kitu,'Ringtone asema huku akidai anaishi maisha ya kifahari ilhali hajasoma

Muhtasari
  • Kupitia  kwenye Instagram yake, Ringtone anahoji kuwa kiwango cha elimu hakiamui mafanikio ya mtu
  • Alitoa mfano wa Akothee ambaye amejenga himaya ya mamilioni licha ya kuwa hana digrii
ringtone apoko
ringtone apoko

Msanii wa nyimbo za injili mwenye utata Ringtone almaarufu Alex Apoko amejigamba kuwa tajiri licha ya kutoenda shule.

Kupitia  kwenye Instagram yake, Ringtone anahoji kuwa kiwango cha elimu hakiamui mafanikio ya mtu.

Kulingana naye, kuwa mchapakazi, kumcha Mungu na kujitolea kumemfanya kuwa mwanamuziki tajiri zaidi Afrika Mashariki.

"NAMESS, SAVARA, NDOVU, NADIA ndio wasani ambao wamesoma sana nchini Kenya, wana shahda kubwa lakini wanateseka kutafuta pesa," Alisema Ringtone.

Alitoa mfano wa Akothee ambaye amejenga himaya ya mamilioni licha ya kuwa hana digrii.

Ili kuthibitisha hoja yake pia alitoa orodha ya wanamuziki wenye digrii lakini wanatatizika kimaisha

"Msanii kama Akothee anaishi maisha ya kifahari ilhali hana digrii, mimi mwenyewe siyuko katika ligi yao lakini masomo sio kila kitu uchapakazi, kumcha Mungu na kujitolea ndi kila kitu

Mimi ni msanii tajiri Afrika kusini," Alisema msanii huyo.