"Jamani muombee Tiffah!" Zari Hassan afichua kuwa bintiye na Diamond anaugua

Muhtasari

•Zari ameeleza kwamba hata madaktari wameshindwa kutambua ugonjwa ambao umeathiri bintiye licha ya ziara zao kadhaa hospitalini.

Image: INSTAGRAM// TIFFAH DANGOTE

Binti pekee wa mwanasoshalaiti Zari Hassan, Tiffah Dangote ni mgonjwa.

Zari ambaye siku za hivi majuzi ameonekana mwenye wasiwasi alitumia ukurasa wake wa Instagram kufahamisha wanamitandao kuhusu afya ya bintiye na kuwasihi wamkumbuke katika maombi yao.

Mama huyo wa watano alisema kwambaTiffah amekuwa akikabiliwa na uchungu mwingi mwilini. Ameeleza kwamba hata madaktari wameshindwa kutambua ugonjwa ambao umeathiri bintiye licha ya ziara zao kadhaa hospitalini.

"Pona haraka. Jamani naomba muombee Tiffah. Madaktari hawawezi kutambua ugonjwa wowote" Zari alisema.

Tiffah ni mmoja wa watoto wawili ambao mwanasoshalaiti huyo mzaliwa wa Uganda alipata na staa wa Bongo Diamond Platnumz wakati walikuwa katika mahusiano.