Zuchu ajitetea dhidi ya madai ya kwenda kinyume na Basata

Muhtasari

•Zuchu amejitokeza na kukana madai yaliyokuwa yakienezwa kwenye mitandao, kwamba alienda kinyume na chama cha kusimamia waimbaji nchini humo Basata.

Zuchu-posing-2
Zuchu-posing-2
Image: Hisani

Msanii maarufu nchini Tanzania,Zuchu amejitokeza na kukana madai yaliyokuwa yakienezwa kwenye mitandao  ya kijamii, kwamba alienda kinyume na chama cha kusimamia waimbaji nchini humo Basata.

Hii imetokea baada ya kuchapishwa kwa video ambayo ilikuwa inaenezwa kwenye mitandao kijamii.

Kwenye ukurasa wake wa instagram, Zuchu ametoa taarifa ya kukanusha madai iliyokuwa analimbikiziwa kwamba alitumia maneno machafu kwenye kituo kimoja cha Televisheni

"Siku hizi za Karibuni, nimekua nikiona hii video ya mahojiano tuliyofanya mwaka jana, mimi Na Mtangazaji @thisisaaliyaah ikisambaa na watu wachache wakijaribu kupotosha maana ya mazungumzo yaliyofanyika" alisema Zuchu 

Alisema kuwa amesajiliwa na chama cha Basata na haoni maana ya kuvunja sheria ambazo zinawaongoza wao kama wasanii wa Tz.

"Neno nililotumia Hapo Ni neno “Mtambo “ mimi ni msanii niliesajiliwa na @basata.tanzania Hivo najua kanuni na sheria elekezi .Pia mimi ni balozi ninawakilisha Taasisi Kubwa... kwa akili timamu siwezi kutumia lugha yoyote ya matusi ya wazi kwenye Chombo cha habari."

Aliendelea kuomba radhi kwa mashabiki wake kwa uvumi ulioenezwa kupitia kanda hio ya video.

"Niombe radhi na nitoe pole kwa jamii na mashabiki zangu wote mliokerika na upotoshaji huu .Na naomba Mpuuzie upotoshaji huu Unaoendelea,"