Milly Wajesus awapa ushauri wanandoa

Muhtasari

• Milly Wajesus alitaja ndoa yao kuwa ni ndoa ya  baraka na kuwaomba wanandoa kuwa watu wenye  uaminifu katika ndoa zao

• Ndoa ni jambo zuri lililowekwa na Mungu. Namshukuru Mungu ambaye ametusaidia katika ndoa yetu

Kabi Wajesus na Milly Wajesus
Kabi Wajesus na Milly Wajesus
Image: INSTAGRAM// MILLY WA JESUS

Milly Wajesus amejitokeza wazi kuzungumza  kuhusu mahusiano yake  na Mumewe Kabi Wajesus.

Kupitia ukurusa wake wa Instagram, Milly Wajesus alitaja ndoa yao kuwa ni ndoa ya  baraka na kuwaomba wanandoa kuwa watu wenye  uaminifu katika ndoa zao. 

Milly Wajesus alijitokeza na kuthibitisha kwamba ndoa inaendelea vyema, na kuwapa motisha wanaopanga kufunga  ndoa hivi karibuni. Akitaja mfano wa ndoa yao kuwa kielelezo tosha.

"Ndoa ni jambo zuri lililowekwa na Mungu. Namshukuru Mungu ambaye ametusaidia katika ndoa yetu. Tunaposema kazi za ndoa sio kwa sababu tumezielewa zote bali ni kwa sababu tunajua aliyeanza kazi njema ndani yetu ni mwaminifu kuikamilisha licha ya kutokamilika kwetu." alisema Milly 

Wapenzi hao wawili mara  nyingi huweka wazi mahusiano kwenye mitandao ya kijamii. Alhamisi, Mally alichapisha ujumbe wa kusherekea ndoa yake akitaja mume wake kuwa bora wakati alipokuwa akisherekea ndoa  yao

"Leo nataka kumshukuru Mungu kwa zawadi ya ndoa na upendo wa maisha yangu. Kwa wanandoa Mungu awape msaada wake katika ndoa yenu. Daima mfanye Yeye kuwa kitovu cha muungano wenu."