Terence Creative asifia matatu iliyopewa jina la Mhusika wake 'Kemikali'

Muhtasari

โ€ขTerence Creative furahia baada ya kuona matatu iliyochorwa picha yake na maandishi ya maigizo yake.

Terence Creative
Terence Creative
Image: Hisani

Muigizaji Lawrence Macharia almaarufu Terence Creative ameonyesha furaha isiyo na kifani baada ya kuona matatu iliyochorwa picha yake huku ikitumia misemo ambayo yeye hutumia katika maigizo yake.

Terence  alijitosa katika ulingo wa sanaa mwaka jana, baada ya kutoa filamu iliyokuwa  ikieleza  jinsi matapeli walivyokuwa wakiibia watu hasa  jijini Nairobi. Filamu iliojulikana kama 'Kemikali'

Kupitia ukurusa wake wa  Instagram, alionyesha furaha yake kwa kuchapisha video hio iliyokuwa imechora picha yake na misemo ambayo kwa muda  amekuwa akitumia kwenye ulingo maonyesho yake.

"Ndoto Hutimia . Pongezi kubwa kwa hili...  zaidi ya matatu 10 kote nchini zinatumia chapa ya Terence Creative."  alisema Telence 

Baadhi ya misemo ilikuyokuwa imechapishwa kwenye matatu ni ikiwemo; Kemikali, Ngamwaya na Weka fine.

Kulingana naye video hiyo ilichukuliwa wakati alikuwa safirini  kuelekea  uwanja Jomo Kenyatta.