Mwanamuziki Justina Syokau '2020' ataja sababu zake kummezea mate Ringtone Apoko

Muhtasari

•Justina amekiri kwamba  anavutiwa sana na bidii ya Apoko katika kazi ya usanii huku akimhakikishia raha tele iwapo atakubali kumuoa. 

•Amesema kuwa kuna wanaume wengi ambao wamejitolea kumuoa iwapo Ringtone hataonyesha nia yoyote ya kumchukua kama mke.

•Amesema miongoni mwa sifa ambazo anaangalia sana kwa mchumba ni urefu pamoja na utanashati

Justina Syokau
Justina Syokau
Image: HISANI

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Justina Syokau almaarufu kama 'Twendi Twendi' amesisitiza kwamba yeye ndiye mke bora kwa msanii mwenzake Ringtone Apoko.

Akiwa kwenye mahojiano na Mpasho, Justina alieleza kwamba 'hajamcrushia' Ringtone ila wote wawili wanavutiana.

Justina amekiri kwamba  anavutiwa sana na bidii ya Apoko katika kazi ya usanii huku akimhakikishia raha tele iwapo atakubali kumuoa. Hata hivyo amesema itamlazimu Apoko kupunguza mdomo iwapo wataishi pamoja.

"Sijamcrushia. Ata yeye alisema ako single na anataka Justina. Mimi tu ndio nawezana na yeye nyumbani kwake Runda.Mimi tutafanya P.E kwa hiyo nyumba itii.Kwanza niliona ako na kiwanja moto. Iko sawa kwa githaa (tendo la ndoa). Ringtone ni msanii mwenye bidii. Ukiangalia nyimbo zake zinasonga vizuri. Ni mtu mzuri katika hali yake ya kawaida. Yeye anaongea sana kweli, lakini tukioana lazima atapunguza mdomo juu wanawake wawili hawawawezi kuishi katika nyumba moja" Justina alisema.

Mwanamuziki huyo hata hivyo amemtahadharisha Apoko kwamba iwapo atasuburi muda mrefu zaidi bila kumyakua huenda akapatia nafasi mmoja wa wanaume wengi wanaommezea mate.

Amesema kuwa kuna wanaume wengi ambao wamejitolea kumuoa iwapo Ringtone hataonyesha nia yoyote ya kumchukua kama mke

"Akikosa kuhudhuria sherehe ya kuadhimisha kuzaliwa kwangu sina shida naye.  Kuna watu wengi wananipigia wananiambia Apoko akishindwa na kazi sisi tupo.  Wanaume ni wengi wanajitolea wananiambia Apoko akishindwa wamejitolea kunioa. Si mmoja, ni wengi lakini Ringtone ndiye nimepatia kipaumbele" Alisema.

Justina amekiri kwamba anatamani kuolewa tena baada ya kukaa bila mchumba kwa kipindi cha miaka nane tangu alipotengana na mumewe.

Amesema miongoni mwa sifa ambazo anaangalia sana kwa mchumba ni urefu pamoja na utanashati. Amesema mchumba wake lazima awe na sura ya kupendeza ili aweze kujivunia kuwa naye