Zari akana madai ya Tiffah kuwa Diamond ndiye alimnunulia kitanda

Muhtasari

•Zari Hassan amechapisha video yenye wameshiriki mazungumzo na  mtoto wake wa kike Tiffah Princess.

•Bintiye Zari anasikika akidai kuwa  babake Diamond ndiye alinunua kila kitu kwenye nyumba yao.

ZARI-DIAMOND-PLATNUMZ-5-e1502092497365(1)
ZARI-DIAMOND-PLATNUMZ-5-e1502092497365(1)
Image: Hisani

Mwanashalaiti na mfanyibiashara mashuhuri kutoka Uganda Zari Hassan na ambaye anaishi Afrika Kusini amechapisha video inayoonyesha akishiriki mazungumzo na  mtoto wake wa kike Tiffah Princess.

Katika video ambayo Zari alichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram , Tiffah anasikika akidai kuwa  baba yake Diamond ndiye alinunua kila kitu kilicho kwenye nyumba yao.

Mtoto huyo wa miaka sita alidai kwamba Babake  ni tajiri wa kupigiwa mfano, huku akieleza kwamba ata kitanda alichokilalia kilinunuliwa na Diamond.

Tiffah pia amasema anamini wazazi wake,Zari na Diamond wanapendana kwa sababu wao hutembeleana kila.

Tiffah ambaye alifuzu kuingia darasa lingine siku chache zilizopita alisherehekewa sana na wazazi wake kufuatia hatua hiyo.

"Niombee kisha unipe nafasi, fumba macho ulale, naenda kuoga," Zari alimwambia Bintiye Tiffah. Mazungumzo yalianza baina ya Zari na Tiffah ambapo Tiffah alimjibu mamake kwa kusema,

"hii ni nafasi yangu yote. hiki ndicho kitanda changu.Unakumbuka baba alikinunua?" alisema Tiffah Kufuatia kauli hio ya mtoto wake Zari alijibu kwa kusema, "Babako yako hakuwahi kununua kitanda hiki" Zari alimwambia Tiffah 

Tiffah aliongeza kwamba chochote kiko kwa chumba chao babake ndiye amenunua na akuonyesha kubadilisha mawazo yake.

"Baba yangu ana pesa nyingi sana..hapana yeye ndiye alimenunua kila kitu nyumbani"