Mtangazaji wa Radio Jambo Mbusii azungumzia suala la kujiunga na siasa

Muhtasari

•Mtangazaji huyo alikiri kwamba vijana wengi wamekuwa wakimshinikiza kuwania viti mbalimbali vya kisiasa jijini Nairobi.

•Mtangazaji huyo pia alisema huwa anapata msukumo wa maisha kutoka kwa mke wake na watoto wake watatu.

Mtangazaji Daniel Githinji Mwangi almaarufu kama Mbusii wakutana na Rais Uhuru Kenyatta katika ikulu mnamo 2017.
Mtangazaji Daniel Githinji Mwangi almaarufu kama Mbusii wakutana na Rais Uhuru Kenyatta katika ikulu mnamo 2017.
Image: MAKTABA

Mtangazaji wa kipindi cha Mbusii na Lion teketeke kwenye Radio Jambo Daniel Githinji Mwangi Mwangi ameweka wazi kwamba hatakuwa anajitosa kwenye siasa licha ya umaarufu wake mkubwa nchini hasa miongoni mwa vijana.

Akiwa kwenye mahojiano na Churchill, mtangazaji huyo alikiri kwamba vijana wengi wamekuwa wakimshinikiza kuwania viti mbalimbali vya kisiasa jijini Nairobi.

Baba huyo wa mabinti watatu alieleza kwamba dini yake ya Rastafari kwa kawaida huwa haihusishi na siasa.

"Rasta haihusiani na siasa zozote. Kwa ground mavijana wananiambia hata naweza kusimama Embakasi Mashariki, nikiangalia hivi Embakasi Mashariki naona hapana. Wengine wanasema nisimame Embakasi Magharibi, lakini huwezi simama. Wacha tu nikae maisha yangu yawe taratibu tu" Mbusii alisema.

Mtangazaji huyo pia alisema huwa anapata msukumo wa maisha kutoka kwa mke wake na watoto wake watatu.

"Siwezi penda wapitie maisha ambayo nimepitia. Kila siku nikiamka asubuhi huwa naambia Mungu wasikose ya kula, wasikose kuvaa. Huwa namuomba  anipatie yao tu wasikose" Mbusii alisema.

Alifichua kwamba amekuw kwenye ndoa na mke wake kwa takriban miaka 14. Walipatana kwa mara ya kwanza wakati alikuwa anafanya kazi ya uigizaji katika shule ambayo mkewe alikuwa anasomea.