"Nataka nipate mume mzungu na mwenye pesa"Rose Muhando asema

Muhtasari

•Alifichua kwamba anafurahi maisha anayoishi na amejitolea katika huduma yake ya  injili   na mara nyingi usafiri kueneza injili hio,kutokana na hilo anasema ni ngumu kutulia wenye ndoa. 

Rose Muhando
Rose Muhando
Image: hisani

Mwanamuziki wa injili kutoka nchi ya Tanzania Rose muhando amefunguka kuhusu mambo anayotaka mwaka huu wa 2022.

Kupitia ukurusa wake wa Instagram alifichua kwamba anafurahi maisha anayoishi na amejitolea katika huduma yake ya  injili   na mara nyingi husafiri kueneza injili,kutokana na hilo anasema ni vigumu kutulia kwenye ndoa.  

Kulingana naye alisema kuolewa kutarudisha huduma yake nyuma, hivyo hayuko tayari kuingia kwenye ndoa.

Muhando ambaye ni mama wa watoto watatu  anasema anataka mwanamume mzungu mwenye pesa.

"Yesu nitendee.. Ombi langu mwaka huu nataka nipate mume mzungu na mwenye ela" alisema Rose Muhando.

Isitoshe aliwambia mashabiki wake wanaweza kutuma maombi yao kwa chochote wangetaka Mungu awatendee mwaka huu na angewasaidia kwa maombi.

"Unaweza nitumia na wewe challenge yako ya Ombi lako huku ukiandika ombi lako unalotaka Mungu akufanyie mwaka huu 2022" alidokeza.