Wakati mmoja nilipigana na Papa Shirandula-Njoro afichua

Muhtasari
  • Alifichua katika mahojiano kuwa kabla ya Papa kumpa nafasi kwenye kipindi hicho aliwahi kuwa makang
  • Alidai Kwamba Papa Shirandula alibadilisha maisha yake kuwa bora zaidi na ndiyo maana baada ya kifo chake Kenneth aliamua kujiita 'Njoro Shirandula' ili urithi wake uendelee kuishi
NJORO 3
NJORO 3

Kenneth Gichoya almaarufu Njoro ni mmoja wa watu wengi wwalionufaika kupitia kipindi cha Papa Shirandula, na kuinuka kutoka kiwango kimoja hadi kingine kwa sababu ya marehemu Charles Bukeko almaarufu Papa Shirandula.

Alifichua katika mahojiano kuwa kabla ya Papa kumpa nafasi kwenye kipindi hicho aliwahi kuwa makanga.

Alidai Kwamba Papa Shirandula alibadilisha maisha yake kuwa bora zaidi na ndiyo maana baada ya kifo chake Kenneth aliamua kujiita 'Njoro Shirandula' ili urithi wake uendelee kuishi.

Aliwekeza pesa nyingi alizolipwa kutokana na onyesho hilo na zingine alizopata kama MC wa hafla katika mali isiyohamishika na hiyo ndiyo inamuingizia mapato baada ya onyesho kumalizika.

Kenneth alifichua kwa mzaha kuwa kuna wakati ambapo walipigana na Papa Shirandula baada ya kunywa maji yake wakati wa safari.

Waligombana na kupigana hadi mtu akawatenganisha. Hata hivyo, hilo halikuwafanya kuwa maadui kwa sababu baadaye walijicheka wenyewe kwa kuwa wao ni watu wadogo na hata kujumuika pamoja siku hiyo hiyo.

"Tulishikana mangumi, lakini jioni tulikuwa tukisikiza rhumba pamoja!Mimi, Nilikunywa maji yake kwa basi tukitravel. Aliniwekelea, naminikamwekelea! Akaanza kutoa damu," Alizungumza Njoro.

Kenneth pia alizungumzia jinsi alivyokuwa karibu na Papa hadi alitaka kuacha onyesho baada ya baadhi ya watu kupanga kuchukua nafasi ya Njoro.

Walikuwa marafiki waaminifu kwa kila mmoja kwamba kifo cha Papa kilikuwa kitu kigumu kwa Kenneth kukubali.