Mwanamuziki mashuhuri kutoka Tanzania Rehema Chalamila almaarufu Ray C ameshauri akina dada hasa ambao wanapenda vileo kuwa wangalifu wanapokuwa kwenye eneo la burudani na wapenzi wao.
Amesema hayo baada ya video ya uchi iliyokuwa ikienezwa kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa ilikuwa ya mwanahabari mmoja wa kike wa Bongo.
Msanii huyo amewashauri wanadada kuwa makini wakati wanatembea kwenye maeneo ya burudani hasa sehemu zilizowekwa camera.
Kulingana naye. wanadada wanapaswa kutafuta wataharamu wa kuwafunza jinsi ya kutumia simu kutambua maeneo ambayo camera zimefichwa.
"mkiwa mtandaoni jaribuni pia kujifunza mengine kupitia mtandao sio mnashinda instagram tu...kwa kifupi wanadada wenzangu hebu tafuteni wataalam wa kuwasaidia kupakua programu ambazo zinaweza kubaini sehemu zimefichwa kwnyee vyumba vya burudani mnavyoingia na waubani wenyu" alieleza Ray C
Isitishe, hakusahau kuwapa onyo wanadada wanapenda kubugia pombe hadi kutojimbua na kufanya mambo wasiotarajia kuyafanya kwa akili zao timamu.
"Hii ni kwa wale wanadada wanapenda Hennesy wewe shambulia Hennesy za watu mpaka unafika kwenye chumba hata akili ya kuchunguza camera huna hapo ndipo utajua hujui.