Msanii wa nyimbo za injili Loise Kim ajitosa kwenye ulingo wa siasa

Muhtasari
  • Haya yanajiri baada ya MC Jessy kutangaza kuwa amejiunga na chama cha UDA rasmi
Loise KIm
Image: Instagram

Msanii wa nyimbo za injili za Kikuyu Loise Kim kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook, ametangaza kwamba amejitosa kwa siasa.

Loise amesema kwamba atawania kiti cha kuwakilisha wanawake kaunti ya Kiambu.

Alitangaza haya baada ya kuwauliza wakazi wa KIambu kujitokeza kwa wingi wapige kura na kujisajili kwa ajili ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu ujao.

Kujitosa kwake Loise kumeongeza idadi ya wasanii na watangazaji ambao wameweka wazi kuwa watawania viti tofauti katika uchaguzi wa Agosti.

Haya yanajiri baada ya MC Jessy kutangaza kuwa amejiunga na chama cha UDA rasmi.

Je kwa nini wasanii wengi wamejitosa katika uwanja wa siasa, mwaka huu kuliko miaka ile ingine yote? Ni swali ambalo mashabiki wao wamesalia nalo, bila ya kupata jibu.

Baada ya wanamitandao kuona ujumbe na tangazo lake Loise walitoa hisia tofauti kuhusu hayo.