Briana aeleza eneo walikutana na Harmonize na penzi likakolea

Muhtasari

•Briana, ameeleza eneo  ambalo  walikutana mara kwanza  na mwanamuziki huyo na wakazama kwenye penzi

•Kulingana na Briana , walipatana na harmonize mara ya kwanza kwenye eneo la burudani nchini Sydney na wakaanza kuzungumza lakini mwaka  2021 ndio alizuru nchi ya Tanzania.

Harmonize na Briana
Harmonize na Briana
Image: istagram/briana

Mpenzi wa Harmonize anayetambulika kama Briana, ameeleza eneo  ambalo  walikutana mara kwanza  na mwanamuziki huyo na wakazama kwenye penzi.

Kulingana na Briana , walipatana na harmonize mara ya kwanza kwenye eneo la burudani nchini Sydney na wakaanza kuzungumza lakini mwaka  2021 ndio alizuru nchi ya Tanzania.

Harmonize mwaka jana alijitokeza na kueleza kiini cha kukosana na wapenzi wake, huku akidai mahusiano yake mengi huvunjwa na aliyekuwa mwajiri  wake wazamani  Diamond Platnumz.

Hivi majuzi harmonize amekuwa akionekana  na Briana kwenye tamasha mbalimbali huku mashabiki wake wakiMpongeza  kwa mahusiano yake na mzungu.

Harmonize ambaye aligura lebo ya Wasafi inayomilikiwa na Diamond Platnumz, na  kuanzisha lebo yake ya Konde gang siku za hivi majuzi  lebo yake imefikiana na country Boy kuondoka kwa kile walisema ni msanii huyo alikatisha muktaba wake.