'Haya yanatokea aje kwa wanawake?'Boniface Mwangi auliza baada ya kufichua makanga waliomnyanyasa mkewe

Muhtasari
  • Kuna baadhi ya wale ambao wamezoea kuwanyanyasa wanawake na hata wengine kuwashika  visivyo endapo wanapanda matatu
  • Mwanaharakati Boniface Mwangi ameshiriki kisa ambapo mkewe Njeri alihangaishwa na makanga wa Matatu

Ni tabia ambayo baadhi ya makanga wamejifunza kuwafanyia wanawake kwani hawana saurti yeyote au nguvu ya kubishana nao.

Kuna baadhi ya wale ambao wamezoea kuwanyanyasa wanawake na hata wengine kuwashika  visivyo endapo wanapanda matatu.

Mwanaharakati Boniface Mwangi ameshiriki kisa ambapo mkewe Njeri alihangaishwa na makanga wa Matatu.

Anasema wababe hao walimgusa mkewe isivyofaa na kuendelea kuwarushia matusi.

Bonnie alishiriki video ya wakali hao ambao waliendelea kuwatusi baada ya tukio hilo. Walimpa changamoto kuchukua video ya Matatu na hata kuipeperusha kwenye TV.

"Nchi hii ilienda kwa mbwa, nilikuwa natembea na mke wangu kwenye barabara ya Kangundo dakika chache zilizopita, mlishaji wa chini akiwa na fulana ya mistari alimgusa alipouliza kwa nini wanaanza kurusha matusi na kushikana sehemu zao za siri. kwa kina kwamba wanahisi kutoguswa! Hii inatokeaje kwa wanawake?" Bonnie aliandika.

Mwanaharakati huyo aliwataka wanawake kubadilishana uzoefu wao katika mikono ya wapiga debe wa aina hiyo.

Swali kuu ni je umewahi nyanyaswa na makanga na ulichukua hatua ipi, au baadhi yao ambao wana tabia kama hii wanapaswa kuchukuliwa hatua ipi?