•Aliuliza , Diamond Platnumz kuhusu kugura kwa mmoja wa wasanii tajika kwenye lebo ya wasafi na kusema alimjibu anayetaka kuondoka na aondoke muziki wa Bongo anaujua.
•Mwaka jana Ravyaan alifungua lebo yake, jambo ambalo lilionekana kama njia ya kufuata Harmonize ambaye alimtangulia kuondoka kwenye lebo hio
Mheshimiwa kutoka nchi ya Tanzania na mwandani wa karibu wa msanii Diamond Platnumz, Mkubwa Fella amejitokeza na kueleza kuna msanii mwingine anatarajiwa kugura Wasafi.
Mkubwa Fella alikuwa katika ziara ya kuzindua bendi ya Yamoto, ambayo alieleza nia yake ni kukuza vipaji vya vijana ambao bado hawajajulikana kwenye ulingo wa burudani.
Aliuliza , Diamond Platnumz kuhusu kugura kwa mmoja wa wasanii tajika kwenye lebo ya wasafi na kusema alimjibu..." anayetaka kuondoka na aondoke muziki wa Bongo anaujua".
"mfano mzuri nilimuliza Naseeb, bwana vipi na huyu anayeondoka vipi,akasema mzee Fella Bongo naijua" alidokeza Mkubwa Fella.
Kupitia kauli hiyo kumekuwa na tetesi hasa kwenye mitandao ya kijamii ya nchini Tanzania kwamba Ravyaan anatarajiwa kugura lebo ya Wasafi.
Mwaka jana Ravyaan alifungua lebo yake, jambo ambalo lilionekana kama njia ya kufuata Harmonize ambaye alimtangulia kuondoka lebo ya Wasafi.
Fella alisema kuondoka kwa wasanii kwenye lebo yoyote ile ni kuonyesha kukomaa kwa wanamuziki huku akisema nia yake ni kukuza talanta za vijana chipukizi.