'Nitarudia mpaka yesu arudi,' Vera Sidika amjibu shabiki aliyesema haya kumhusu

Muhtasari
  • Mwanasosholaiti maarufu nchini Vera Sidika anafahamika kwa masiha yake ya kifahari ambayo anaishi
Image: INSTAGRAM// VERA SIDIKA

Mwanasosholaiti maarufu nchini Vera Sidika anafahamika kwa masiha yake ya kifahari ambayo anaishi.

Vera alivuma sana mitandaoni mwaka jana baada ya kutangazia mashabiki wake kwamba anatarajia kifungua mimba wake na msanii Brown Mauzo.

Vera amebarikiwa na mtoto ambaye ana urembo wa kipekee, na ,ambaye aliadhimisha miezi 3, siku ya Alhamisi 20, Januari.

Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram Vera amempa mmoja wa mashabiki wake jibu baada ya kusema kwamba hajawahi jua kama watu maarufu uwa wanarudia mshipi wa nguo.

Kulingana na mwanasosholaiti huyo mshipi huo alinunua elfu mia mbili, ambao ni wa Gucci, na atarudia mpaka ile siku yesu atarudi.

"Kumbe celebrity hurudi rudi belt lol," Shabiki aliuliza.

Vera alimjibu kuwa;

"Nilinunua mshipi huo wa Gucci elfu mia mbili,nitarudia mpaka Yesu arudi."