'Usikate tamaa,'Aliyekuwa mwanahabari wa Switch asema huku akifanya kazi ya makanga

Muhtasari
  • Mtangazaji huyo wa zamani, Robert Ouma alienda kwenye mitandao wa kijamii siku ya Alhamisi kusimulia uzoefu wake wa matatu kufikia sasa
Aliyekuwa mwanahabari wa Swich TV Robert Ouma
Image: Hisani

Aliyekuwa mtangazaji wa Switch TV amelazimika kuchukua wadhifa mpya kama makanga wa matatu ili kujikimu, kufuatia kuachishwa kazi kwa wingi katika kituo kinachomilikiwa na Msalaba Mwekundu Desemba 2021.

Mtangazaji huyo wa zamani, Robert Ouma alienda kwenye mitandao wa kijamii siku ya Alhamisi kusimulia uzoefu wake wa matatu kufikia sasa, jambo lililowashangaza mashabiki wake.

Katika video inayozunguka kwenye mitandaoni mwanahabari huyo wa zamani anaonekana mwenye sura ya kupendeza anapomaliza kufanya shughuli zake za kila siku katika matatu inayopitia njia ya Rongai-Nairobi.

Baada ya kupakia video hiyo alikuwa na haya ya kusema;

"Tunafunga funga kazi hapa, ni saa mbili na dakika ishirini na tisa. Ofisi ni jina tu lakini pesa ni tamu tu. Kesho pia ni siku majaliwa,Mtu afanye anachoweza kufanya maanake ndivyo hali ilivyo."

Ouma alipakia video nyingine kwenye mitandao ya kijamii, huku akiwashauri mashabiki wake wasikate tamaa, katika kila jambo.

Mnamo Desemba 2021, Mwenyekiti wa Switch TV, Sahil Shah alitangaza kuwa shirika la habari lingehama kutoka utangazaji wa hewani ili kuzingatia mkakati unaolenga zaidi kidijitali na kukaribia kutekelezwa 2022 kutokana na kubadilisha mwelekeo wa soko.

"Kwa tabia ya falsafa yetu ya msingi ya kuwa msikivu kwa mahitaji ya vijana na kwa nia ya kuwa jukwaa la vyombo vya habari kwa kizazi kipya, Switch Media imefanya uamuzi wa kujenga mkakati mpya kuhusu kuwa digital-kwanza," Shah alisema.