Nyota Ndogo awakemea wanaomweka kwenye machapisho kuhusu Wamarekani wanaowaua wapenzi wao Wafrika

Muhtasari
  • Nyota Ndogo awakemea wanaomueka kwenye machapisho kuhusu Wamarekani wanaowaua wapenzi wao Wafrika
nyota ndogo
nyota ndogo

Msanii kutoka mkoa wa pwani Nyota Ndogo amezua hisia tofauti tena mtandaoni, hii ni baada ya kuwaonya Wakenya waziwazi dhidi ya kumweka kwenye kila chapisho la kijinga kuhusu Wamarekani kuwaua wapenzi wao weusi, ili wathibitishe kwake kwamba Wamarekani ni watu wabaya.

Nyota Ndogo alisema kuwa, unyanyasaji wa nyumbani kwa kawaida hutokea kila mahali duniani, hata hapa Afrika, Waafrika Wanaume huwaua wapenzi wao wa kike, ni kitu kinachotokea, na Wakenya na Waafrika, kwa ujumla tunapaswa kuacha kuwahukumu Wamarekani, na kwa pamoja tusimame dhidi ya unyanyasaji wa nyumbani.

Msanii huyo alisema kuwa ni jamii iliyokamilika, na pia kuna Wamarekani wazuri na Wamarekani wabaya kama ilivyo barani Afrika, na kwake yeye na mumewe Nielsen wapo katika hali nzuri na hajawahi kudhalilishwa wala kunyanyaswa na Nielsen.

"Nimeshangaa kutagiwa kwa ujinga unao endelea Dunia nzima. Sasa mwanamke ameuwawa na mume wake mzungu uko ulaya

Pole kwa Familia ya mfiwa. Sasa ndio watu wanitag eti wazungu ni wanyama wanauwa watu Mara ooh waschana waafrika wanakimbilia wazungu wanaenda kuuwawa.

Sasa mimi munanitag ya nini? Even here in Africa blacks are killing too their fellow women na wanatupa kwa river.....was Tirop the marathon runner married to a mzungu???

It's a matter if being careful whom you choose to be your life partner mbona visa vingi tu ni vile lazima mzungu akifanya kitu lazima mututie sote ndani.

Binadamu sote ni Binadamu. Na haya yanatokea ulimwengu ni. Kila siku mauwaji i ya wapenzi yanatokea humu humu. WAPELEKE UJINGA UKO."