Siezi amini niko 'single'-Harmonize asema baada ya kutemwa na mpenzi wake

Muhtasari
  • Mwimbaji kutoka Tanzania Rajab Abdul anayejulikana zaidi kama Harmonize, hivi majuzi alichukua hadithi zake za Instagram kuelezea upande wake wa maisha
Harmonize na Briana
Harmonize na Briana
Image: INSTAGRAM// HARMONIZE

Kuachana na mtu unayempenda mara moja si rahisi kwa kila mtu. Huu ni wakati ambao hisia ya hatia inatawala ndani ya moyo wako, hutaki kumuumiza mtu uliyempenda sana lakini kumpenda hata baada ya kuwa ngumu zaidi kuliko kuvunja moyo wa mtu.

Mwimbaji kutoka Tanzania Rajab Abdul anayejulikana zaidi kama Harmonize, hivi majuzi alichukua hadithi zake za Instagram kuelezea upande wake wa maisha.

Harmonize alifichua kuwa anaishi maisha mazuri lakini aliongeza kuwa hayajakamilika bila mwanamke kuwa naye.

Harmonize amekuwa na mahusiano kadhaa lakini hayajakuwa yakifaulu, hivi karibuni aliachana na Kajala Masanji na kuanza uhusiano mpya na Briana ambaye walionekana wakiwa pamoja. wakati Harmonize alipokuwa katika ziara nchini Marekani.

Leo Harmonize kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram alipakia ujumbe ukionyesha kuwa sasa yuko single na pia wote wawili wameacha kufuatana kwenye mitandao ya kijamii ya Instagram.

Harmonize katika ujumbe wke alisema kwamba hawezi amini kwamba amekuwa Single tena.

"Siezi amini niko single tena," Aliandika Harmonize.