Diamond azungumzia Ravyaan kuondoka Wasafi

Muhtasari

• Diamond Platnumz alizungumzia kiwango cha ubora wa  Ravyaan na kuwapongeza wote waliomsaidia kumsajili kwenye lebo yake.

• Kilichosalia kwa wafuasi wa Ravyaan nikuona akitangaza siku rasmi ya kuaga Wasafi kama alivyofanya Harmonize.

 

Ravyaan na Diamond Platnumz
Ravyaan na Diamond Platnumz
Image: Hisani

Siku chache zilizopita kumekuwa na uvumi kuhusu hatma ya mwanamuziki Ryvanny katika lebo ya Wasafi. 

Wiki jana Mkubwa Fella akizungumza na kituo kimoja cha radio nchini Tanzania akigusia  jambo hilo ingawa hakutaja jina la  msanii aliyekuwa ananjama ya kuondoka Wasafi.

Alisema, aliuliza Diamond kuhusu msanii anayetaka kuondoka na Diamond akamjibu kuwa... "muziki wa Bongo flava naujua na anayetaka kuondoka naondoke".

Wikendi hii kwenye uzinduzi wa  lebo ya Ravyaan, Diamond Platnumz alizungumzia kiwango cha ubora wa  Ravyaan na kuwapongeza wote waliomsaidia kumsajili kwenye lebo yake.

Diamond ambaye alikuwa amevaa suti ambayo inasawiana na  Ravyaan alieleza safari ya Rayvanny tangu wamsajili na mambo aliyoafikia akiwa kwenye lebo hiyo.

"kwanza niwashukuru wote, najua kuna mambo mengi yanaendelea duniani  lakini mwenyezi Mungu katuponya..kwa upande wangu kabla sijaenda mbali na washukuru  Babu Talle na Madihi  kwa sababu  chimbuko la Ravyaan  lilikuwa  pale. Lakini baada ya kukutana naye nikaona ana kipaji na kwa kipindi kile  nilikuwa naanzisha lebo yangu ya  Wasafi, tuliongea na wakubwa wake tukawaomba watupe Ravyaan," alisema Diamond

Alieleza wazi kwamba Rayvanny tangu wamsajili amekuwa akionyesha ubora wake kwa kila kazi yake.

"kuanza kufanya kazi na Ravyaaan alikuwa  akikua kwa kasi,, hadi kufikia hapa, Ravyaan Mimi nakupongeza sana kwa sababu  sio tu mimi ila Wasafi nzima kwa kuifanya itambulike zaidi,"  

Kilichosalia kwa wafuasi wa Ravyaan nikuona akitangaza siku rasmi ya kuaga Wasafi kama alivyofanya Harmonize.