Illuminati walinipa pesa, lakini hawakutaka nimtaje Yesu kwenye nyimbo zangu-Jimmy Gait afunguka

Muhtasari
  • Kulingana na maoni yake alisema kuwa kila mtu ana haki ya kufanya maamuzi yake kulingana na majimbo yake na jinsi anataka kuyafanikisha
jimmygaitsuit1
jimmygaitsuit1

Leo Jimmy Gait ambaye ni mmoja wa magwiji bado wangali hai katika tasnia ya muziki ya kenya alikuwa na mahojiano ya kustaajabisha na mojawapo ya chaneli nchini.

Alielezea uzoefu wake alipokuwa mwanachama wa kikundi ambacho kinaaminika kufadhiliwa  na watu wanaoaminika kuwa Illuminati.

Aliendelea kukiri jinsi Illuminati ilimpa mamilioni ya pesa na ndio maana aliweza kufikia ndoto yake ya kazi ya muziki.

Aidha, alisema kutoungwa mkono na serikali na makampuni mengine ambayo yanashindwa kutoa ridhaa ya wasanii wanaofanya vizuri ndiyo kumewalazimu mastaa wengi kujiunga na Illuminati kwa sababu wanaogopa kufilisika.

Kulingana na maoni yake alisema kuwa kila mtu ana haki ya kufanya maamuzi yake kulingana na majimbo yake na jinsi anataka kuyafanikisha.

Pia alifichua kuwa wanachama wa Illuminati hawakutaka tu, aimbe nyimbo, bali hawakutaka ataje jina Yesu kwenye nyimbo hizo.

"Illuminati walinipa mamilioni ya pesa, lakini hawakuwa wanataka nitaje jina la Yesu kwenye nyimbo zangu, lakini walitaka nyimbo nzuri sana

Pia walikuwa tayari kunipa lebo ambayo ingefanya vibao vynagu vienee sana, lakini niliona hapana nikakataa," Jimmy Alidai. 

Usemi wake JImmy unajiri siku chache baada ya msanii Magix Enga kukiri jinsi alivyojiunga na kikundi hicho na yale alipitia baada ya kutoka.

Je kulingana na Jimmy Gait anatafuta kiki au vipi, kama vile wanamitandao wengi wanasema Enga anatafuta kiki.