'Tuheshimiane' harmonize awambia waliosema ameachwa

Muhtasari

•Kondeboy amejitokeza wazi na kueleza bado ana mpenzi wake mzungu, Briana

•Briana ambaye alizuru nchi ya Tanzania mwezi Desemba, 2021 na kuonekana kwenye tamasha mingi na kipenzi chake harmonize.

•Kupitia kurusa wake wa instagram, Harmonize ameweka mambo wazi kuwa hawajachana na mpenzi huyo wake na kuwaonya wanaoenesha uvumi wakome.

 

Harmonize
Harmonize

Mwanamuziki kutoka nchi ya Tanzania Almaarufu Kondeboy amejitokeza wazi na kueleza bado ana mpenzi wake mzungu, Briana.

Ikumbukwe siku ya Jumamosi msanii huyo alichapisha ujumbe kwenye Instastory kwamba ameachwa.

Jambo lililochukuliwa na wanamitandao kuwa kweli kwani wapenzi hao walikuwa wameacha kufuatiliana kwenye mitandao ya kijamii hasa  ukurusa wa instagram.

Briana ambaye alizuru nchi ya Tanzania mwezi Desemba, 2021 na kuonekana kwenye tamasha mingi na kipenzi chake harmonize.

Kupitia kurusa wake wa instagram, Harmonize ameweka mambo wazi kuwa hawajachana na mpenzi huyo wake na kuwaonya wanaoenesha uvumi wakome.

“sipo single tuheshimiane” alisema Harmonize.

Ni hivi majuzi habari za harmonize zimekuwa zikienea kwenye mtandao wa kijamii kwamba mahusiano mengi yake huwa hayadumu kwa muda mrefu.

Harmonize ambaye aligura Lebo ya Wasafi na kuanzisha lebo yake ya Konde Gang  ameonekana  kujituma  zaidi kuhakikisha  lebo yake imejulikana dunia nzima.