Rapa wa Marekani ameshinda kesi aliyopeleka kortini mwaka wa 2019 dhidi ya Tasha K,ambapo alidai mwanablogu huyo alitunga madai kumhusu kwenye mtandao wake wa kijamii.
Cardi B alimshtaki Tasha K kwa kuweka video ambayo alikuwa anaeleza kuwa Cardi B ni Kahaba ambaye alijihusisha na dawa za kulevya na aliambukizana magonjwa ya zinaa.
Kulingana na Mtandao wa TMZ, Cardi alidai mwanablogu huyo alitunga uwongo mbaya kumhusu jambo ambalo halikuwa rahisi kujitetea ila kupeleka mahakamani.
Baada ya kusikizwa kwa wiki moja, makahakama imempata Tasha K na hatia ya makosa matatu na kuamuru kulipa Cardi pauni milioni 1.25 kama uharibifu wa jumla na pauni 250,000 kwa gharama za matibabu.
Kabla Cardi kuwasilishe kesi hiyo kortini mwaka wa 2019 alikuwa amepigia simu Tasha na kumtaka aondoe video hio kwenye ukurasa wake lakini alidinda kufanya hivyo.
Hakimu alisema fidia zote za adhabu ambazo Tasha anaweza kumdai Cardi zitaamuliwa katika kesi ya baadaye.