Siwezi enda kumtafuta mwanamume huo ni umalaya-Rose Muhando aweka wazi kwa nini anamtaka mzungu tajiri

Muhtasari
  • Rose Muhando aweka wazi kwa nini anamtaka mzungu tajiri
Rose Muhando

Wiki jana msanii wa nyimbo za injili kutoka Tanzania Rose Muhando alivuma Mitandaoni baada ya kutangaza kwamba ana mtaka mzungu tajiri ili awe mume wake.

Akiwa  kwenye mahojiano na wanahabari msanii huyo aliweka wazi kile alichokuwa anamaanisha na kusema kwamba anamtaka mzungu tajiri.

"Ndoa ni kitu ambacho unajaliwa, siwezi enda kuitafuta au kulima shambani siwezi enda kumtafuta mwanamume, huo ni umalaya, ila nitamwambia mungu," Muhando alisema.

Aidha msanii huyo alisema kwamba kumchagua mzungu ni chaguo lake, na wala sio mzungu ngozi bali mwenye hela.

"Choice yangu, nimechagua choice yangu. Mbona mzungu anaoa Maasai? Sijaomba mzungu ngozi, nimeambia mungu nipe mzungu mwenye pesa. Si anioe, anipe hizo pesa nikahubiri injili.

Si azeeke kisha anampa Mbwa hela, alete hapa. Kwani nimevunja sheria ya nchi? Kati ya Amri kumi za mungu nimekosea ipi? Basi hiyo imeisha."