Mbona uharibu wakati wako na mpenda wanawake-Wanamitandao wamuuliza Zuchu

Muhtasari
  • Wanamitandao watoa hisia tofauti kuhusu uhusiano wake Diamond na Zuchu
Diamond Platnumz na Zuchu
Diamond Platnumz na Zuchu
Image: INSTAGRAM

Kwa muda sasa uvumi umekuwa ukienea kwamba staa wa bongo Diamond Platnumz na Zuchu wana uhusiano wa kimapenzi.

Ni uvumi ambao Juma Lokole alithibitisha, wakati wa mahojiano na wanahabari wa Tanzania.

Juma, amebaini kuwa Diamond na Zuchu wamekuwa kwenye mahusiano kwa takribani mwezi mmoja.

“Unajua ukweli mapenzi hayafichiki na ni vizuri tuweke mambo wazi…Zuchu na Diamond wana mahusiano...Hivi sasa ni mwezi mmoja ”.. alisema Juma lokole.

Vile vile walijaribu kumpigia simu Diamond ilikuthibitisha habari hizo ambapo alikataa kuchukua simu yake huku akiwandikia arafa kwamba amesikia wanachotaka kumuliza.

Hivi majuzi Zuchu alijitokeza hadharani na kushukuru mpenzi wake ambaye jina lake alilibana kwa kumnunulia mdoli mkubwa Ikumbukwe Mwezi uliopita, Diamond na Zuchu walionekana pamoja.

Wanamitandao wametoa hisia tofauti kuhusu uhusiano wake Diamond na Zuchu, huku wengi wakisema kwamba anaharibu wakati wake.

Doreen Mukami: Sasa hii fisi inataka kuharibia haka kasichana maisha .... Zuchu unafikiria wewe ndiye mzuri ama mrembo kuliko hao baby mamas wengine .

Melodious Karani: Diamond baba yao kila msichana poooh

Musa Yusuph: Zao mbwembwe tuuu na hawadumishi mapenzi yao

Kitutus Dota: Shda yenu n hii,hamuezi acha mtu atumie manhood yake kwa amani mpaka mumfatilie😏

Mercy Mulanda: Mimba loading 🙈 huyu huwa halali class😂😂

Carl Khivan: Sasa tunangoja mimba na mtoto mwingine, Diamond naye ni nani.