•Nadia Mukami ameeleza kushangazwa na baadhi ya marafiki zake baada ya wao kuona video ya mpenziwe Arrow Bwoy iliyokuwa ikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii
•Arrow boy alionekana akimvisha kipusa moja pete, kinyume na matarajio ya mashabiki wake kwani walifahamu Nadia kuwa mpenzi wake ambaye wanatarajia kufunga ndoa
Mwanamuziki Nadia Mukami ameeleza kutamaushwa na tabia za baadhi ya watu waliokuwa karibu naye hasa baada ya video kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha mpenziwe Arrow Bwoy akimvisha pete mwanamke.
Arrow boy alionekana akimvisha kipusa moja pete, kinyume na matarajio ya mashabiki wake kwani walifahamu Nadia kuwa mpenzi wake ambaye wanatarajia kufunga ndoa naye.
Nadia hakufumbia macho swala hilo alizungumzia madai hayo, ambapo alikiri alitumia mtandao wa Google kubaini kama kinachosemwa ni kweli ama ni uvumi tu.
"Mwanamume alitoka kwa mwanamke... Nimeona ile video ya @arrowbwoy nikaanza kuzigoogle Tafadhali nisaidie dondoo zingine kwenye sehemu ya Maoni," alidokeza.
Ambapo Arrow Boy alimjibu kwa kusema Nadia aliomuonya dhidi ya kumpa msongo wa mawazo.
"Nilikushow usi ni stress ntavuka chama Next unaona sasa" alisema Arrow boy.
Kutokana na majibizano baina ya wapenzi hawa wawili, Nadia amedokeza waliokuwa marafiki wake karibu wameanza kumpotelea.