BASATA yakutanisha Alikiba, Diamond na Harmonize

Muhtasari
  • BASATA latarajia kukuwakutanisha wasanii sifika wa nchi hio kwenye uzinduzi anaofanyika tarehe 28 Januari 2022
  • Baraza hilo ambalo limekuwa limesitisha tunzo hizo kwa muda limetangaza kupitia ukurasa wao wa instagramu kwamba wanarudisha tunzo hizo
Harmonize,Alikiba na Diamond
Harmonize,Alikiba na Diamond
Image: Hisani

Baraza la Sanaa Nchini Tanzania, BASATA latarajia kukuwakutanisha wasanii sifika wa nchi hio kwenye uzinduzi anaofanyika tarehe 28 Januari 2022.

Baraza hilo ambalo limekuwa limesitisha tuzo hizo kwa muda,lilitangaza kupitia ukurasa wake wa instagram kwamba wanarudisha tuzo hizo.

Kulingana nao, tuzo hizo zitashirikisha wasanii kutoka ndani ya nchi pekeeTanzania.

Wasanii  ambao wamepokea mwaliko rasmi ni;Alikiba, Diamond, Harmonize,Nandy, Zuchu na miongoni mwa wengine.

Alikiba anatarajiwa kukaa meza moja na Diamond jambo ambalo si la kawaida kwani  wasanii hao wawili  hawajawai kutana kwenye tamasha yoyote. 

Isitoshe, itakuwa mara  ya kwanza Diamond kukutana na Harmonize baada ya kugura Lebo yake ya WCB na kutengeneza Lebo yake mpya.

Harmonize mwezi jana alipokuwa akirejea nchini Tanzania, alieleza yote yaliyomkumba wakati alikuwa akifanya kazi na Lebo  ya Diamond.

Kilichoshangaza  zaidi kwenye mialiko hio , Diamond na Zuchu ndio wamepokea mwaliko rasmi kutoka timu wasafi.