Harmonize:Ali Kiba lazima aimbe kwenye hafla yangu ya kuasi ukapera

Muhtasari

•Harmonize alichapisha video fupi iliyokuwa ikicheza wimbo mpya wa Alikiba unaoitwa ‘Utu’ huku akiambatinisha na ujumbe kwamba siku ya kuvisha pete  mpenzi wake lazima King Kiba atumbuize mashabiki wake.

Harmonize na Alikiba
Harmonize na Alikiba
Image: INSTAGRAM

Mwanamuziki Maarufu nchini Tanzania Harmonize ameonyesha heshima kwa mwanamuziki mwenzake wa Bongo Flava Alikiba kwa kumpongeza kwa kazi nzuri anayofanya kwenye tasnia ya Muziki wa Bongo.

Kupitia ukurasa wake Wa instagram, Harmonize alichapisha video fupi iliyokuwa ikicheza wimbo mpya wa Alikiba unaoitwa ‘Utu’ huku akiambatinisha na ujumbe kwamba siku ya kuvisha pete  mpenzi wake lazima King Kiba atumbuize mashabiki wake.

“Mtu amwambie mkongwe, mfalme Alikiba lazima aimbe kwenye usiku wa kumvisha pete mchumba wangu, huu muziki mzuri sana,” Harmonize aliandika.

Hivi majuzi wanamuziki hao walionekana wakisafiri kwa ndege moja, jambo  ambalo wanamitandao walilijadili kwa  wiki kadhaa.

Ikikumbukwa wasanii waliosajiliwa na wasafi Record hawana  mkabala mzuri  na Ali Kiba.

Swali ambalo wengi wanajiuliza  kwa sasa ni kwa  nni Harmonize amekuwa na mkabala mwema na Ali kiba ikikumbukwa wakati alikuwa Wasafi hawakuwa wanazungumza.