'Kuna maisha baada ya mapenzi,'Paula Kajala awashauri mashabiki

Muhtasari
  • Hizi hapa hisia za mashabiki baada ya Paula Kajala kusema haya kuhusu mapenzi

Mapenzi ni ya muhimu maishani mwa kila mmoja, hasa wakati umempata mtu akufaaye maishani mwako.

Kuna baadhi ya watu ambao wamekataa tamaa kwa ajili ya mapenzi na kuambia moyo yao ifanye kazi ya kusukuma damu na wala sio kupenda.

Paula Kajala alifahamuka sana mitandaoni baada ya kuwa mpenzi wake staa wa bongo Rayvanny, huku uhusiano wao ukikashifiwa sana na mashabiki.

Paula na Rayvanny wamekuwa wakivuma mitandaoni baada ya uvumi kuibuka kwama wawili hao wameachana.

Wawili hao hawajaweka wazi kama wameachana, ilhali wameacha kufuatana kwenye mitandao ya kijamii ya instagram huku wakifuta picha zao wakiwa pamoja kwenye mitandao hiyo.

Paula, aliwashauri mashabiki wake kuendelea na maisha yao hata baada ya mapenzi.

"Kuna maisha baada ya mapenzi 😒😒😒."

izi hapa baadhi ya hisia za mashabiki baada ya ushauri wake;

rebecajumajohn: Wewe mzuri utapata mwingine 😍😍

lucytemu79: 😢😢😢😢 elimu ndy kila kitu paula mapenz yapo tu

ashlit49: Umepata mwengin uturuki hongera paula

jumamenja3: Kimeumana Leo ulikuwa unatukera haya endelea xaxa cc bdo tupo single sijui ww umeingza nn baada ya dudu

comediengondora: Huwezi ku achika hivihivi ina onekana una mimba tu 😂 sababu rayvanny hawezi kuku acha kibwege😂

Kulingana na mashabiki wengi ni kuwa hizi ni kiki kwani wasanii wengi wamezoea kutumia mapenzi yao kama kiki ili vibao vyao vifume.

Je ni kiki au ukweli wa waili hao?