Msemaji wa Yanga atishia kugura Tanzania ikiwa hawatashinda taji

Muhtasari

•Msemaji wa Yanga, Haji Manara amejitokeza na kusifia ubora wa timu  ya Yanga huku akikiri mwaka huu timu ya hio lazima inyakue ubingwa wa ligi ya Tanzania

•Aliwai kuwa msemaji wa timu ya simba  amekuwa akipiga  vijembe timu hio kwa kueleza wakati umefika Yanga  kuinua kombe la ligi hio ya Tanzania

Msemaji wa Yanga Haji Manara
Msemaji wa Yanga Haji Manara
Image: hisani

Kama ilivyokawaida mpira wa kandanda kuambatana na hisia za aina yake baina ya mashabiki wa timu kinzani. Msisimko huu na mihemko ambayo inahusishwa na mchezo huu imeufanya uwe na mashabiki wengi duniani..

Msemaji wa Yanga, Haji Manara amejitokeza na kusifia ubora wa timu  ya Young Africans huku akikiri mwaka huu timu hiyo lazima inyakuwe ubingwa wa ligi ya Tanzania.

Haji, ambaye aliwai kuwa msemaji wa timu ya simba  amekuwa akipiga  vijembe timu hio kwa kueleza wakati umefika Yanga  kuinua kombe la ligi hio ya Tanzania.

Kupitia  mahojiano katika kituo kimoja cha habari nchini  Tanzinia, Haji alisema Yanga imekaa miaka nne bila kushinda kombe lolote, jambo ambalo si sawa kabisa ikizingatiwa timu hiyo inawafuasi wengi nchini humo.

 Simba ilipokezwa kichapo cha mbwa na timu ya limbukeni Kagera. Manara amekiri kama Yanga haitashinda Kombe hilo mwaka huu atahama nchi yaTanzania na kwenda kuishi mbali.

"Yanga imekaa miaka nne bila ubingwa, mashabiki hawawezi subiri, na ndio maana nasikia vichekesho na kero.. maisha ya kukariri, Yanga ikikosa Ubingwa mimi nahama nchi hii," alisema Haji.

Mashabiki wa Simba wameonekana kukerwa na maneno ya Haji, huku wakisema wanachojua ni kuwa  Yanga haitaweza kumaliza kileleni.