Muthoni Drummer Queen atambulisha mtoto wake kwa Mashabiki

Muhtasari

•Furaha ilidhihirika kwa Rapa Mashuhuri nchini Kenya Muthoni Drummer Queen na Mpenzi wake Musa Omusi baada ya kutambulisha mtoto wao wa kwanza mbele ya mashabiki wake.

•Vilevile, aliweka wazi jina la mtoto  wake kuwa ni  Manjano Ndonga Musosi, jina ambalo ni la marehemu Babake huku Musosi ni Mchanganiko wa jina lake na la mpenzi wake.

 

Muthoni the Drummer Queen na familia yake
Muthoni the Drummer Queen na familia yake
Image: hisani

Tunaanza kwa kumpongeza Muthoni the Drummer Queen kwa kujifungua mtoto wake wa kwanza.

Kama ujuavyo Furaha ya mzazi nikuona mwanawe anakua vyema  bila changamoto zozote.

Hii ndio furaha iliodhihirika kwa Rapa Mashuhuri nchini Kenya Muthoni The Drummer Queen na Mpenzi wake Musa Omusi baada ya kutambulisha mtoto wao wa kwanza mbele ya mashabiki wake.

Kupitia ukurusa wake wa Instagram, Muthoni alipakia video huku akionyesha Kitoto chao kichanga.

Vilevile, aliweka wazi jina la mtoto  wake kuwa ni  Manjano Ndonga Musosi, jina ambalo ni la marehemu Babake huku Musosi ni Mchanganiko wa jina lake na la mpenzi wake.

Ikumbukwe ni hivi majuzi tulichapishwa habari za ujauzito wa Muthoni, Na sasa amejifungua kifungua mimba wake.