Napenda wanaume-Michelle Ntallami

Muhtasari

• Baada ya penzi la Michelle Ntarami na Makena Njeri kuingiwa na zogo kisha kusambaratika.

• Ntalami ametangaza habari njema hasa kwa wanaume kwamba yuko tayari kuchumbiwa na wao.

• Amekuwa akidaiwa kuwa mwanachama wa Kikundi cha LGBTQ ameonakana Alhamisi kujitetea kwa kukiri kuwa yuko tayari Kutoka kimapenzi na mwanamme yeyote

 

Michelle Ntallami
Michelle Ntallami
Image: instagram/michelle

Mapenzi bora ni yale ya kumwonyesha unayemwita Mpenzi unamwamini na kumuenzi liwe jua au Mvua.

Baada ya penzi la Michelle Ntallami na Makena Njeri kuingiwa na zogo kisha kusambaratika, Ntalami ametangaza habari njema hasa kwa wanaume kwamba yuko tayari kuchumbiwa na wao.

Ntalami ambaye amekuwa akidaiwa kuwa mwanachama wa Kikundi cha LGBTQ ameonakana Alhamisi kujitetea kwa kukiri kuwa yuko tayari Kutoka kimapenzi na mwanamme yeyote.

Hii ni baada ya Kuachwa na  Makena Njeri Mwaka jana. Makena Alidai kwamba Ntalami alikuwa akitoka kimapenzi na watu wengine Kinyume na makubaliano yao, na hivyo kuamua kumpa Talaka.

Kauli ya Ntallami imewadia baada ya kuulizwa swali na Mashabiki wake kwenye ukurusa wa Instagram kama anaweza chumbiana na Wanaume.

Kutokana na kauli yake amewavutia wafuasi wengi baada ya kugundua anapenda wanaumme.

“Mimi ni androsexual maana; Mtu ambaye anavutiwa sana na wanaume au nguvu za kiume. (Andro ni kiambishi awali cha Kigiriki kinachomaanisha mwanamume). Pia najua nimewafundisha nyie jina jipya.” Alisema Ntallami.